Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe ametangaza kusitisha mpango wa vijana wa chama hicho kwenda Dodoma kuzuia
Mkutano Mkuu wa CCM ili kuepusha maafa ambayo yanaweza kutokea. Badala yake,
Mbowe amesema wataendelea kusaka haki ya kufanya mikutano ndani na nje ya
nchi.
Sambamba na uamuzi huo, chama hicho
kimetaka viongozi sita wa Baraza la Vijana (Bavicha) wanaoshikiliwa na Jeshi la
Polisi kuachiwa mara moja.
Mbowe alitoa tamko hilo jana wakati
akizungumza na wanahabari jijini Arusha, katika mkutano wa mameya na wenyeviti
wa halmashauri 18 zinazoongozwa na Umoja wa Katiba ya wananchi (Ukawa).
Sababu za kusitisha
Mbowe alisema wamewataka vijana wa Chadema nchi nzima ambao walianza kujiandaa kwenda Dodoma kuisaidia polisi kuzuia mkutano huo wa Julai 23 kutokwenda kwa sababu polisi wamepewa maagizo ya kuwapiga na kuwajeruhi, hivyo wao hawataki kupambana nao.

“Nawataka vijana wote wa Chadema
waliokuwa wanajiandaa kwenda Dodoma wasitishe na wasubiri maelekezo mapya ya
Chadema,”alisema Mbowe.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema wana taarifa Jeshi la Polisi
limejipanga kuwanyima dhamana viongozi wa Bavicha hadi baada ya mkutano wa CCM,
ingawa viongozi wote wa chama hicho hawana hofu ya kukaa mahabusu.
Aliwataka vijana hao kutokwenda
Dodoma na wawaache CCM waendelee na mkutano wao kwa kuwa Chadema haina hofu na
mkutano wa chama hicho, bali walitaka dunia ione jinsi polisi wanavyofanya kazi
kwa maelezo ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya nchi.
“Wakati sisi tunazuiwa kufanya
siasa, Rais anafanya siasa, Waziri Mkuu anafanya siasa, mawaziri wanafanya
siasa, wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya siasa jambo ambalo si sahihi,” alisema.
Alisema lengo la Bavicha
kwenda Dodoma ni kuchoshwa na uonevu wa kuzuiwa kufanya mikutano ya ndani na
hadhara wakati CCM wanaendelea na mikutano yao.
“Waliona pengine itakuwa busara
washinikize polisi kuona maagizo yao ya kuzuiwa mikutano yanatekelezwa kwa
wote,” alisema.
Alilitaka jeshi la polisi kufanya
kazi kwa kufuata taratibu kwa kutoa haki sawa kwa wote, kwa kuruhusu vyama
vyote kufanya mikutano yao.
Apinga tamko la Mwigulu
Kuhusu tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuhusu mikutano hiyo, Mbowe alisema hawakulielewa tamko hilo la Rais, kuwa mikutano ambayo imezuiwa ni ya hadhara na maandamano na si ya ndani.

Alisema mikutano ya ndani ya chama
hicho imezuiwa kwani Chadema Wilaya ya Kahama walikuwa na mkutano wa ndani wa
uchaguzi ambao umezuiwa.
Alisema mkutano wa ndani na
wabunge wa Chadema mkoani Shinyanga ulizuiwa na pia mahafali za Vijana wa Vyuo
Vikuu wa Chadema (Chaso).
“Lakini wakati haya yanafanyika,
CCM waliendelea na mikutano yao na mahafali yao,” alisema.
Alisema Chadema itaendelea kudai
haki ya mikutano na maandamano katika mahakama za ndani na nje ikiwamo ya
Afrika ya Mashariki.
Viongozi wa madiwani
Katika mkutano wa wenyeviti wa halmashauri 18 zinazoongozwa na Chadema, Mbowe alisema Calist Lazaro, Meya wa jiji la Arusha amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa madiwani wa Chadema nchini.
Katika mkutano wa wenyeviti wa halmashauri 18 zinazoongozwa na Chadema, Mbowe alisema Calist Lazaro, Meya wa jiji la Arusha amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa madiwani wa Chadema nchini.
Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob
alichaguliwa kuwa katibu wa madiwani wote wa chama hicho na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Tarime, Moses Matiku alichaguliwa kuwa mnadhimu wao. Wote hao
watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu Chadema.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent
Mashinji alisema katika mkutano huo wenyeviti hao wamepatiwa elimu juu kuongoza
vyema halmashauri zao ili kuchochea maendeleo.
“Siku mbili za mkutano huu tumekaa
na kuweka mikakati bora ya kuhakikisha halmashauri zinazoongozwa na upinzani
zinafanya vizuri,”alisema.

No comments:
Post a Comment