Mtu huyo kwa jina Datta Phuge aliwahi kununua shati mojawapo
ghali zaidi duniani kwani lilikuwa la dhahabu.
Dhababu ya shati hilo inasemekana hapo 2013 ilikuwa kilo tatu
3kg na liligharimu $250,000.
Polisi wamewakamata wanaume wanne kuhusiana na mauaji ya Datta
Phuge.
Tetesi
ni kuwa huenda si shati lake la dhahabu wala vito na vyombo vya dhahabu
anavyovaa vilivyomchongea kuawa bali wanashuku ulikuwa mzozo wa kifedha.
Phuge alikuwa akifanya biashara ya kukopesha watu fedha kwa
faida na huenda alikosana na baadhi ya wateja wake.
Katika uhai wake aliwahi kuulizwa kwanini anapenda kuvalia na
kujinakshi kwa dhahabu chungu nzima, jibu lake ni hili....Hiyo ndio imekuwa
ndoto yangu tangu zamani, kama vile watu wengine hupenda magari ya kifahari
kama vile Audi ,Mercedes, nami napendelea mng'aro wa dhahabu''

No comments:
Post a Comment