Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia mahafali ya wanafunzi
waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ) yaliyokuwa
yamepangwa kufanyika jana mchana chuoni hapo jijini Dar es Salaam, ambapo
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alikuwa amealikwa na wanafunzi kama mgeni
rasmi.
Mahafali hayo yalizuiwa jana saa 6
mchana ikiwa ni saa mbili kabla ya muda kuanza
Tangazo lililobandikwa chuoni hapo
na kushuhudiwa na wanahabari likiwa linamnukuu Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
hicho, Profesa Apollinary Kamuhabwa liliwataka wanafunzi hao kutoweka
mikusanyiko ya aina yoyote chuoni hapo.
Profesa Kamuhabwa kupitia tangazo
hilo aliwaonya wanafunzi hao kutojihusisha na masuala ya siasa wawapo chuoni
kama ilivyo kwa watumishi wa umma.
Jitihada za waandishi wa habari
kuzungumza na uongozi wa chuo hicho ili kupata ufafanuzi ziligonga mwamba baada
ya kuelezwa kuwa hawakualika mkutano na waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment