Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana July 30 2016 ameendelea na ziara yake
katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa Singida.
Mkoani Tabora, Rais Magufuli
alizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na
Ziba na alifanya mikutano ya hadhara Igunga na Nzega ambako amewahakikishia
wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika
Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.
Katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu
kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa
wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza
kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.
Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli
alisema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka
nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa
Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge
Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga
Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega
Mkoani Tabora.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na wabunge wa Singida
No comments:
Post a Comment