
MAJAMBAZI wanne wamevamia kijiji
cha Benaco kilichopo katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa muda wa saa tatu
ambapo wamefanikiwa kupora Sh milioni 2.4 na simu ambazo hazikujulikana idadi
yake kwa mfanyabiashara mmoja wa huduma ya M-Pesa.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
Kagera ambaye pia ni ofisa upelelezi wa polisi mkoa huo, Abel Mtagwa, alisema
kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo majambazi hao walikuwa
na silaha moja ya kivita aina ya SMG.
Alisema kuwa wakati majambazi
wakijiandaa kuondoka eneo hilo walimpiga risasi mwanafunzi wa kidato cha pili
katika shule ya sekondari ya Gankabo Wilayani Kibondo mkoani Kigoma
aliyetambuliwa kwa jina la Nelson Simon (15) na kumjeruhi mguu wake wa kulia.
Mwanafunzi huo amelazwa katika hospitali teule ya Murgwanza iliyopo wilayani
humo.

No comments:
Post a Comment