Mameya wawili wa
zamani wa Rwanda wamehukumiwa kifungo cha maisha jela mjini Paris kutokana na
kuhusika kwao na mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa mwaka 1994.
Octavio Ngenzi na Tito
Barahira walikutwa na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu na pia kusaidia na
kupanga mauaji ya watu wa jamii ya watutsi katika vijiji vyao upande wa
Mashariki mwa Rwanda.
Ni kesi ya pili
kuamuliwa nchini Ufaransa dhidi ya watu wanaotuhumiwa kushiriki katika mauaji
hayo ya kimbari.Octavien Ngezi alikuwa Meya wa Kabarondo. Tito Barahira alikuwa
mtangulizi wake katika nafasi hiyo.
Katika hukumu ndefu na
ya kuchosha, wanasheria wa Ufaransa walifikia muafaka kuwa wanaume hawa wawili
walichangia pakubwa katika mauaji ya kimbari katika eneo la Kabarondo mwezi wa
April mwaka 1994.
Katika mauaji
yaliyotekelezwa kwa ukatili mkubwa mamia ya wanaume, wanawake na watoto
walichinjwa baada ya kutafuta hifadhi katika kanisa la kijiji.
Kwa miaka 22 Kesi
ilikuwa ikiegemea katika ushahidi wa watu walioshuhudia, na upande wa utetezi
ulijitetea kwa kusema kuwa baada ya kipindi hicho kirefu kumbukumbu zilikuwa si
za kuaminika tena na kwa hivyo ushahidi huo si wa kufaa.
Watuhumiwa hao wawili
muda wote waliendelea kusema kuwa walikuwa watazamaji wa tukio ambalo
wasingeweza kusaidia lolote katika kilichotokea. Lakini mwisho mahakama
ikahukumu kuwa walishiriki katika kupanga na kutekeleza mauaji yaliyolenga
kumaliza watu wote wa jamii ya watutsi.
Sheria za ufaransa
zinazipa haki mahakama za ufaransa kuhukumu makosa dhidi ya ubinadamu na mauaji
ya kimbari hata kama makosa hayo yalitendeka nje ya ufaransa.
Miaka miwili iliyopita
sheria hii ilitumika kwa mara ya kwanza kwa kumuhukumu mnyarwanda mwingine
Pascal Simbikangwa afisa wa usalama ambayae naye alikutwa na hatia ya kushiriki
katika mauaji ya kimbari.

No comments:
Post a Comment