Mwanariadha mlemavu wa
nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela
kwa hatia ya kumuua mpenzi wake.
Pistorius alimuua
mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake huko Pretoria kwenye Valentine’s
Day, miaka mitatu iliyopita – tukio ambalo amekuwa akisisitiza kuwa ni bahati
mbaya kwakuwa alihisi ni jambazi.
Upande wa mashtaka ulisisitiza kuwa mwanariadha huyo na mpenzi wake walijibizana kabla ya tukio hilo.
Mwaka 2014 jaji huyo huyo alimhukumu Pistorious kwa kosa la kuua bila kukusudia lakini mahakama kuu iliibadilisha kesi yake kuwa ya kuua kwa kukusudia na hatimaye hukumu mpya kutolewa Jumatano hii.
Hiyo itakuwa ni hukumu ya mwisho ya kesi hiyo ya miaka kadhaa sasa.

No comments:
Post a Comment