Mke wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani
Donal Trump, Melania, amefuta tovuti yake baada ya vyombo vya habari nchini
Marekani kuanza kutilia shaka ukweli wa baadhi ya madai yake.
Bi Trump amesema tovuti hiyo imefutwa kwa sababu haikuwa
inaashiria wala kuonyesha mambo anayoangazia kwa sasa.
Vyombo vya habari nchini Marekani vilikuwa vimetilia shaka
ukweli wa madai kwamba ana shahada katika usanifu mijengo kutoka chuo kikuu
kimoja nchini Slovenia, kama alivyokuwa ameandika katika wasifu wake mtandaoni.
§
Kitabu kuhusu maisha yake kilichochapishwa mwaka huu kinasema
aliacha masomo baada ya mwaka mmoja kuangazia kazi ya uanamitindo.
Wiki iliyopita,
Melania Trump, alishutumiwa
vikali baada ya hotuba aliyoitoa kwenye Kongamano kuu la chama cha Republican,
kudaiwa kuwa kukopa sana maneno kutoka kwa hotuba iliyotolewa na mke
wa rais wa sasa Michelle Obama katika kongamano la chama cha Democratic miaka
minane iliyopita.
No comments:
Post a Comment