Hillary Clinton amekubali rasmi kuwa mgombezi wa Urais wa
Marekani kupitia chama cha Democratic, huku akisema wakati wa kupambana na
mpinzani wake sasa umeanza rasmi.
Alitoa wito kwa wanachama wote wa Democratic kuungana naye huku
akimkebehi mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump, katika madai
yake kuwa ni yeye pekee anayeweza kuyasuluhisha matatizo ya Marekani.
Alisema kuwa Wamarekani hufanya kazi kwa pamoja kyatatua yote
yanayonufaisha taifa.
Awali, bintiye Chelsea Clinton alikuwa ametoa hotuba na kumsifu
sana mamake. Alisema ni mwanamke ambaye huwa hasahau anawapigania akina nani.
"Watu huniuliza kila wakati, huwa anawezaje kufanya haya?
... ni kwa sababu huwa hawasahau watu anaowatetea," amesema.
"Najua kwa moyo wangu wote kwamba mamangu atatufanya
tujionee fahari."
No comments:
Post a Comment