Wakati anahit na ngoma
kama Mapozi na zingine, Mr Blue alijikuta amesahau kabisa kutongoza.
Anadai
kuwa kutokana na ustaa aliokuwa nao, wasichana wengi walimtaka na yeye
alichokifanya ni kuchagua amtakaye na kumpa mambo. Blue anasema enzi hizo
alikuwa playboy haswaa!
“Kwahiyo unakuta wanakuja wenyewe, leo uko na huyu, kesho uko na
huyu, kesho huyu anakupigia simu anakukumbusha ‘unakumbuka jana tulikuwa wote’
namuambia ahh no sikukumbuki, kwahiyo nilikuwa nao zaidi ya kumi halafu wote
kwa pamoja, huyu anakuja nakuambia hebu subiri nipo na huyu. Na anajua lakini
haondoki, na anaweza akaja nikamuambia ‘wewe huyu rafiki yako nimempenda wewe
ondoka’ anaondoka na kesho anakuja, sijui nilikuwa nimewaroga na kitu gani,
nilifanya upuuzi wa aina nyingi sana,” Blue alikiambia kipindi cha The Playlist
cha Times FM.
Blue anasema miongoni mwao walikuwepo mastaa ambao alidai
wengine asingependa kuwataja.
“Wengi wanajulikana niliwahi kutoka nao lakini pia wasiojulikana
wako wengi kweli yaani wenyewe tu unakuta ukifika maskani unakuta kama nagawa
pesa wamejaa pale.”
Mastaa wanaojulikana aliowahi kuwa nao ni pamoja na Wema Sepetu
na Naj.

No comments:
Post a Comment