Kituo cha runinga mjini Saudia
kilionesha picha za moto mkubwa uliokuwa ukiwaka kwenye maegesho ya magari huku
magari yakiteketea na mwili mmoja wa binaadamu ulionekana karibu yake.
Mpaka sasa hakuna kauli yoyote
iliyotolewa na serikali ya Saudi Arabia kuhusiana na tukio hilo,tukio jingine
limetokea huku mtu mwingine wa kujitoa muhanga akiwa amejiripua katika msikiti
wa madhehebu ya Shia upande wa Mashariki mwa mji wa Qatif, na mripuko wa tatu
umetokea karibu na ubalozi wa Marekani mjini Jeddah.
Askari wawili wa kulinda usalama
wamejeruhiwa katika mojawapo ya matukio hayo.Mpaka wakati huu hakuna taarifa
zozote kuhusiana na kundi lililo husika kupanga na kutekeleza mashambulizi hayo
.Lakini kumekuwa na wasi wasi huenda wapiganaji wa Islamic State wakawa
wanahusika.
Kumekuwa na shutuma kuwa utawala wa
Saudia kuwa sio wa halali na ambapo wamekuwa wakiiushambulia ufalme huo mara
kwa mara katika siku za nyuma.

No comments:
Post a Comment