Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya
Msamaha kwa Wafungwa (Parole), Augustine Mrema amemmwagia sifa Rais John
Magufuli huku akiwataka Watanzania kumpa siku 100 aonyeshe mabadiliko katika
magereza nchini.
Mrema aliyasema hayo jana
alipohojiwa katika kipindi cha Amka Tuongee kinachorushwa na Kituo cha
Televisheni cha Star tv.
“Ni Rais mzuri tuliyempata, ni
mchapa kazi, tumpe muda kwa sababu ndiyo kwanza ana miezi minane, lakini ni
mchapa kazi kiasi kwamba marais wenzake wanatembea yeye anakimbia,” alisema.
Julai 16, Rais Magufuli alimteua
Mrema ambaye ni Mwenyekiti TLP baada ya kumkumbusha ahadi aliyompa wakati wa
kampeni eneo la Himo Kilimanjaro kuwa wasipomchagua kuwa Mbunge wa Vunjo
atampatia kazi.
“Nina uhakika nitafanikiwa kwa
sababu nilipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nilifanya mambo makubwa hadi
nikapewa cheo cha Naibu Waziri Mkuu,” alisema.

No comments:
Post a Comment