Ikiwa zimebaki siku tatu kabla ya Mkutano Mkuu wa CCM kufanyika, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limesema azma yao ya kufanya kikao chao cha kamati ya utendaji mjini Dodoma ipo palepale.
Julai 16, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kikao cha Bavicha hakitofanyika kwa sababu
itakuwa ni mwendelezo wa vurugu zao.
Mkutano Mkuu wa CCM, utakuwa na
ajenda mbalimbali ikiwamo ya Mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete
kumkabidhi kijiti cha uongozi Rais John Magufuli.
Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius
Mwita jana alisema baraza hilo lipo kwenye hatua ya mwisho ya
maandalizi ya kikao hicho kitakachohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 kutoka
mikoa yote.
“Wajumbe wataanza kuwasili kesho (leo) mjini Dodoma. Hatuna wasiwasi na kikao hiki kwa sababu ni cha ndani siyo mkutano wa hadhara, ambao umepigwa marufuku na polisi,” alisema Mwita.
“Wajumbe wataanza kuwasili kesho (leo) mjini Dodoma. Hatuna wasiwasi na kikao hiki kwa sababu ni cha ndani siyo mkutano wa hadhara, ambao umepigwa marufuku na polisi,” alisema Mwita.
Mwita alisema kikao hicho kitakuwa
cha siku mbili kuanzia Julai 20 hadi 21 na kwamba, kitahudhuriwa na mameya na
wenyeviti vijana wa halmshauri zinazoongozwa na Chadema.
Alipotafutwa Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Boniface Jacob ambaye ni mwanachama wa Bavicha kujua kama
atahudhuria kikao hicho alijibu:“Nitakwenda kwa sababu mimi ni kijana, sina
sababu ya kukataa wito wa viongozi wangu wa juu wa Bavicha taifa.”
Kuhusu kauli ya Kamanda Mambosasa,
Mwita alisema polisi ilishatoa maelekezo ya kuruhusu vikao vya ndani.
“Taarifa ya Mambosasa
hatujaishangaa kwa sababu ni desturi yake kujichanganya, leo anasema hivi kesho
vile. Tunamtaka atulie asubiri tumpe taarifa ni wapi kikao chetu kitanyika kwa
njia ya amani,” alisema Mwita

No comments:
Post a Comment