Bingwa
wa mbio za Olimpiki za walemavu, Oscar Pistorius, anaweza kuwa miongoni mwa
wanariadha watakaoshiriki michuano ya Olimpiki, Tokyo, nchini Japan kama
akiomba msamaha kwa jamii ili kuwa sehemu ya mashindano hayo.


Mahakama ya nchini Afrika Kusini ilimhukumu kifungo cha miaka
sita jela kwa kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp, mwaka 2013 kwa kumpiga
risasi nne.
Hukumu hiyo kwa Pistorius ni mara ya pili baada ya awali
kufungwa kifungo cha mwaka mmoja nje kabla ya baadhi ya majaji kugomea uamuzi
huo na kutaka kusikilizwa kesi yake.
Jaji wa kesi hiyo, Thokozile Masipa, alimpa Pistorius nafasi ya
upendeleo na kuwajibika kwa hukumu ya mauaji kwa kifungo cha miaka sita badala
ya miaka 15 kutokana na mazingira ya mwanariadha huyo.
Miaka 15 ni adhabu ndogo ikilinganishwa na kitendo cha mauaji
chini ya sheria ya Afrika Kusini, isipokuwa hakimu anaweza kufanya hivyo baada
ya Jaji kujiridhisha, huenda yanaweza kuwa mazingira ya kutuliza baada ya awali
kuhalalisha adhabu ndogo.
Jaji Masipa anasema kwamba, hakukuwa na sababu ya mwanariadha
huyo awali kupewa adhabu nyepesi ambapo ilisababisha majuto.
Kimsingi kesi hiyo ilikuwa na mazingira ya kipekee kutokana na
kitendo cha mauaji na kuwa miongoni mwa kesi ya kipekee kwa kuwa hayakuwa
maisha ya kawaida yanayoweza kuhusisha kitendo alichokifanya mwanariadha huyo.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa michuano ya Olimpiki nchini
Afrika Kusini, Tubby Reddy, anasema kwamba mwanariadha huyo anaweza kutumikia
mwaka mmoja tu akiwa jela na baadaye kutoka na kuendelea na mazoezi ya kujifua
na michuanoa hiyo.
Reddy anasema kwamba hakutakuwa na tatizo kwa mwanariadha huyo
kurejea kwenye kikosi cha wanariadha watakaokwenda Tokyo kwa ajili ya
kuliwakilisha taifa lake kwenye michuano hiyo.
Anasema kwamba, mwanariadha huyo anatakiwa kurudi na kuomba
radhi kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuishi maisha ya kawaida kama raia mwingine
ndani ya Afrika Kusini na kudai kuwa hakuna sheria inayomzuia mwanariadha huyo
kujumuika na jamii yake.
Pistorius anatakiwa kufanya hivyo kutokana na kuigawa jamii
ndani ya Afrika Kusini kwa kuwa wapo ambao hawatafurahi kwa kitendo cha yeye
kuwa huru lakini wengine watakuwa na furaha.
Reddy anasema kwamba, Pistorius anaweza kutumikia kifungo cha
nje baada ya mwaka mmoja kuwa jela na kuwa na muda mrefu wa kujiandaa kabla ya
michuano hiyo.
Siku ya pili wakati Pistorius akiwa jela na kuelekea hospitali
ya Magereza ya Kgosi Mampuru 11, walionekana baadhi ya watu kuwa na hisia za
hasira juu yake kama vile hawakuwa tayari kumsamehe.

No comments:
Post a Comment