
Koffi Olomide Alikamatwa Jumanne
July 26 2016 nyumbani kwake Kinshasa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa
kike wakati wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi na
baadaye ikawa imeripotiwa kuwa amehukumiwa kwenda jela miezi 18 na adhabu hiyo
kutajwa kuwa haitakuwa na faini.
Taarifa zilizoripotiwa ni kwamba
Koffi Olomide kaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya
miezi 18 aliyohukumiwa awali.
BBC imeripoti kuwa kuachiwa
kwa koffi Olomide kumekuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona
sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya
JKIA.
Pamoja na baadhi ya vyombo vya
habari Afrika kuripoti kwamba Koffi alihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela ,
Promoter wake wa nchini Kenya Jules Nsana amekanusha madai hayo na
kusema kesi dhidi ya Koffi ilikuwa bado iko kwenye uchunguzi na kwamba
baada ya uchunguzi wamebaini hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Koffi
Olomide.
Promoter Jules amesema Olomide
alimpigia simu akamtaka aombe msamaha kwa wakenya wote kwa niaba yake

No comments:
Post a Comment