Kupitia video iliyosambaa katika
mitandao ya kijamii amesema timu nzima ya Psquare kwa sasa imerudi tena pamoja.
Akiwa amevalia kofia ndani ya gari,
video hiyo inamuonesha Okoye ni mwenye kujuta, akisema kuwa anabeba jukumu kwa
yote yaliyotokea.
Peter alikuwa na uhasama na pacha
wake Paul, ambaye ndiye amekuwa akiimba naye kwa zaidi ya muongo mmoja, hali
iliyofanya kugawa kundi hilo.
Kulikuwa na dalili kwamba utengano
wao huo unahatarisha mafanikio ya mapacha hao.
Peter na Paul ambao wanapiga muziki
wa hiphop wametoa nyimbo nyingi zilizovuma ndani ya Nigeria na nchi nyingine za
Afrika.

No comments:
Post a Comment