Mbatia pia alizungumzia hali ya kisiasa
na kidemokrasia nchini na kusema chama chake kimebaini kuwa taifa linaongozwa
kwa matamko ya Rais John Magufuli badala ya kufuata Katiba, sheria na kanuni.
Alisema demokrasia imeendelea
kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa na akatolea mfano
mwenendo wa Bunge ambao alisema licha ya kuwa chombo cha kikatiba chenye
mamlaka kamili ya kujiendesha, limeanza kuingiliwa katika uendeshaji wake kwa
wabunge kunyimwa fursa ya kujadili kwa uwazi masuala ya Watanzania.
Alisema NCCR inakemea matu- mizi ya
nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya
siasa, kuwakamata na kuwaweka rumande viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa
makosa mbalimbali.
“NCCR Mageuzi tunalaani tabia ya
polisi kuwakamata na kuwahoji mara kwa mara viongozi wa kisiasa na kuwashtaki
kwa makosa mbalimbali… vitendo hivi ni ukiukaji wa uhuru na haki za vyama vya
siasa katika kufanya kazi zao,” alisema Mbatia.

No comments:
Post a Comment