Chombo cha anga za juu cha shirika la Marekani la NASA
kilichopewa jina Juno kimetuma picha za kwanza za sayari ya Jupiter.
Moja ya hizo, iliyotolewa na NASA Jumanne inaonesha sayari hiyo
ikiwa imezungukwa na miezi mitatu kati ya miezi yake minne mikubwa.
Miezi inayoonekana ni Lo, Europa na Ganymede. Mwezi huo mwingine
uitwao Callisto hauonekani.
Picha hiyo ilipigwa Jumamosi sayari Juno ilipokuwa inazunguka
sayari hiyo ikiwa umbali wa maili milioni tatu.
Hata katika umbali huo, Shimo Jekundu, lililosababishwa na
dhoruba kali kwenye sayari hiyo karne nyingi zilizopita, linaonekana.
Juno
iliingia katika mzingo wa Jupiter wiki iliyopita na kuanza kuizunguka sayari
hiyo ambalo pia hufahamika kama Zohali au Zozali.
Safari yake kutoka duniani hadi ilichukua miaka mitano.
Juno itachunguza na kupeleleza sayari hiyo kwa miezi 20, lengo
kuu likiwa kusaidia wanasayansi kubaini asili ya sayari hiyo ambayo wanaamini
inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi asili ya mfumo wa jua.
Chombo hicho cha juu kilipokuwa kinaikaribia Jupiter, kamera
zake na mitambo mingine muhimu vilizimwa kuzuia visiharibiwe na miali
nururishi. Baadaye, vilifunguliwa.
Wanasayansi wanatarajia picha za karibu zaidi za Jupiter
zitapokelewa mwezi ujao.
§
Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara
300 zaidi
§
Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja
huko hudumu saa 10.
§
Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.
§
Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.

No comments:
Post a Comment