
Picha ya msichana akimbusu Rais wa
Afrika Kusini, Jacob Zuma imezua utata nchini humo.
Picha hizo zilisambaa Jumatano hii
baada ya msichana huyo kuziweka kwenye mitandao ya kijamii. “We will check the
matter,” alisema msemaji wa serikali Bongani Ngqulunga alipoulizwa kuhusu picha
hizo.
Msichana huyo mwenye miaka 19
anaitwa Lindokuhle Dlamini. Kwenye picha hizo aliandika: He is not just a
blesser, we are inlove and I am grateful for all that he has done for me, much
love. Xo xo.”
Blesser inamaanisha ni mtu mzima
anayehonga wasichana na kuwa na uhusiano nao. Akaunti yake ya Facebook
imefutwa.
Hata hivyo mtoto wa kiume wa rais
huyo, Edward amedai kuwa msichana huyo ni dada yake na kwamba akaunti iliyopost
picha hizo ni feki. Baadhi ya magazeti likiwemo Citizen‚ yamesema yaliambiwa na
wasomaji wake kuwa ni kweli binti huyo ni mtoto wa Zuma.
Hata hivyo Makamu wa Rais wa
Economic Freedom Fighters Floyd Shivambu alikosoa kwa kutweet: Okay cool? What
kind of Grand Fathers and Fathers kiss their Grand Daughters & Daughters
like this? Perverts??”
Serikali bado haijatoa majibu kama
ilivyoahidi.

No comments:
Post a Comment