Alikuwa ameshtakiwa kwa kuwaua
swara watatu katika jimbo la Kaskazini la Rajasthan mwaka wa 1998. Mwaka
uliopita aliachiliwa na mahakama kwa kosa jingine la kumkanyaga na kumuua mtu
asiye na makaazi.
Salman Khan, ni nyota wa filamu
kutoka kundi la waigizaji la India, maarufu Bollywood, ambaye ana sifa ya
kujikuta mashakani mara kwa mara.
Mwaka 1998 alilaumiwa na kabila
moja la Rajasthan kwa kupiga risasi na kuwaua swara watatu wakati alipokuwa
katika shughuli za uwindaji.
Swara
hao wanalindwa kisheria na pia wanasujudiwa na kabila lililoshtaki.
Alikuwa amepatikana na kosa na mahakama ya chini na kuhukumiwa
kifungo lakini sasa ameachiliwa baada ya kukata rufaa.
Mwaka uliopita, nyota huyo anayejipata mashakani mara kwa mara
aliachiliwa na mahakama kwa kosa la kumkanyaga kwa gari mtu asiye na makaazi
alipokuwa akiendesha gari lake.

No comments:
Post a Comment