
Jeshi la polisi mkoani Arusha,
limewaita kwa mahojiano, mbunge wa Karatu,Wilbroad Qambalo, mbunge wa viti
maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso na Mwenyekiti wa halmashauri ya
Karatu,Jubilate Mnyenye kutokana na kupuuza agizo la kutofanya mikutano ya
hadhara katika jimbo hilo.
Mwingine ambaye ametakiwa kwenda
kuripoti polisi ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Bajuta.
Wakizungumza jana baada ya
kukabidhiwa barua za wito wa polisi, Qambalo na Paresso walisema wamestuka
kutakiwa kuripoti ofisi ofisi ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha jumatano.
Parreso alisema,walipokea barua
jana saa sita mchana na kutakiwa kuripoti kwa RCO, saa nane lakini
wakampigia na kumweleza wana ratiba nyingine tayari waende jumatano na
akakubali.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,
Charles Mkombo alipotakiwa kuelezea agizo hilo alisema yupo likizo.

No comments:
Post a Comment