Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za
Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda amempongeza Rais John Magufuli kutokana na
ahadi yake ya kurejesha mali za Waislamu.
Lakini Sheikh Ponda hajakubaliana
na kitendo cha Rais kutoa fedha taslimu kwa ajili ya kuchangia safari za Hija,
akisema mkuu huyo wa nchi angezungumza na wahusika ili kujua matatizo ambayo
fedha hizo zingesaidia.
Sheikh Ponda amesema ahadi hiyo ya
Rais ni ya kuungwa mkono kwa kuwa inaonyesha kujali masilahi ya wananchi,
hususan Waislamu.
Juzi, akihutubia Baraza la Idd el
Fitr jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema atawasaidia Waislamu kurejesha
mali zao na kumpongeza Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakar Zubeir kuwa
alikuwa mstari wa mbele katika kurejesha mali hizo kabla hata hajapewa cheo
hicho.
“Nakumbuka wakati nikiwa Waziri wa
Ardhi, kabla hujawa Mufti, pamoja na viongozi wa Bakwata na wengine, ulifika
ofisini kwangu ukieleza jinsi mali za Waislamu zilivyokuwa zinadhulumiwa.
"Ninafamu pamekuwa na hiyo
tabia ya baadhi ya viongozi wenye mali kuwatumia viongozi wa Bakwata na dini
nyingine katika kuwarubuni na kuingia ubia. Mali hizo baadaye huwa zinapotea
kabisa,” alisema.
“Tujitahidi kwa nguvu zote
kusimamia mali hizi zisije kuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani. Tunapenda
wawekezaji, lakini wanachokiahidi hawatekelezi. Haiwezekani.
“Haiwezekani na wala haikubaliki
kwa watu kwa ujanja wao na wakati mwingine kwa kutumia wanasheria wao kukalia
mali za Waislamu. Mali za Waislamu lazima zirudi na za Wakristo zirudi ili
amani iwepo.”
Sheikh Ponda alisema kwa kauli
hiyo, Rais Magufuli ametambua juhudi ambayo wamekuwa wakizifanya katika
kupigania mali za Waislamu, kama ilivyokuwa katika kupigania kiwanja cha
Chang’ombe hadi kusababisha kesi dhidi yake na wenzake.
“Utakumbuka, tulikuwa na kesi
kuhusu kiwanja cha Waislamu kule Chang’ombe, katika hatua za awali tulishindwa,
lakini baadaye tukakata rufaa na kushinda. Ndiyo sababu ya kuunga mkono kauli
hii ya Rais,”alisema Sheikh Ponda.
Akizungumzia msaada wa Rais
Magufuli kwa ajili ya Hija, alisema hiyo ni ruzuku muhimu, lakini Rais angekaa
na Waislamu wamweleze mambo ambayo ni muhimu zaidi ili uwekezaji wake uwe na
manufaa zaidi.
Alipoulizwa ni mambo gani ni muhimu
zaidi, Sheikh Ponda alisema ni masuala ya elimu na afya ambayo Serikali
ikisaidia baadaye yatapunguza mzigo mkubwa kwake

No comments:
Post a Comment