Bwana Blair amesisitiza kwamba hakuipotosha Uingereza kuingia
katika vita hivyo, ingawa ameomba radhi kwa familia zilizifiwa na ndugu zao
wakati wa vita hivyo.
Tonya Blair amesema anaamini kwamba ulikuwa ni uamuzi sahii wa kumuondoa
kiondongozi wa zamani wa Iraq marehemu Saddam Hussein, na kwamba angeweza
kuchukua uamuzi kama huo wakati huu.
"Wacha tuwe wazi kuhusu uamuzi. Inatokana na kilichotekea
huko Mashariki ya kati. Na ninaamini kwamba Iraq ingepata utulivu na Mashariki
ya Kati pia ingepata utulivu. Kuhusu tathimini yangu kwa yale yanayoendelea
huko mashariki ya kati ni mapambano makubwa, kuondoa siasa za kidini na kuweka
siasa zinazojumuisha watu wote,kuvumiliana, na kuvuliana dini za watu wengine.
Na uamuzi huo ilikuwa na nia ya utawala unajenga uchumi sio uchumi wa ufisadi.
Kwa sasa nafikiri hivyo ni vitu viwili, watu wanapambana eneo zima la Mashariki
ya kati. Na Iraq chini ya Saddam haina nafasi." alisema
viongozi waandamizi katika maamuzi nchini Uingereza wameanza kurusha
lawama kwa mshirika wao Marekani juu ya uamuzi uliochukuliwa mwaka 2003 dhidi
ya vita vya Iraq kutokana na athari za uamuzi huo kuzidi kuonekana miaka kumi
na nne baadaye.
Mapema wiki hii, Uingereza uchunguzi uliofanywa na John Chilcot
umeegemea kuelekeza mashambulizi makubwa juu ya maandalizi,utekelezaji na
matokeo ya vita vya Iraq.
Jenerali Tim Cross, mmoja kati ya viongozi waandamizi wa jeshi
nchini Uingereza kushiriki katika mipango vita hivyo,Alisema Marekani inapambua
jeshi la Iraq na chama cha Ba'ath zilivyoingia vitani bila kufuata ushauri.
Naye Jeremy Greenstock,balozi wa Uingereza Balozi katika Umoja
wa Mataifa alinukuliwa akisema kwamba Marekani iliisukuma jeshi la Uingereza
mapema mno, na kuongeza kusema kwamba wachunguzi wa umoja wa mataifa wanapaswa
kutumia muda zaidi kuchunguza masuala ya kemikali na silaha za kibaiolojia
zilizotumika katika vita vya Iraq .
Alistair Campbell,alikuwa mkuu wa kitengo cha mawasiliano wakati
wa utawala wa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, amesema kwamba
Wamarekani hawatekelezi makubaliano yaliyofikiwa kabla kama walivyotarajiwa .

No comments:
Post a Comment