Dereva huyo ambaye alikuwa amembeba mpenzi wake ndani ya gari
lao alisimamishwa na polisi katika eneo la Falcon Heights kisa , taa moja ya
upande wa nyuma wa gari lake ilikuwa imepasuka.
Alipoulizwa leseni yake akanyosha mkonowe kana kwamba
anaichukuwa upande wa nyuma na polisi huyo akampiga risasi 4 papo hapo.
Mpenziwe Lavisha Reynolds, na mwanawe walikuwa naye ndani ya
gari hilo.
Bi Lavisha Reynolds, alikuwa akipeperusha moja kwa moja tukio
hilo kupitia kwenye mtandao wa Facebook.
Japo mkanda huo umefutwa kwenye Facebook ,watu wamejitolea kuuchapisha
tena na tena.
Mkanda huo unamuonesha Philando Castile akivuta pumzi yake ya
mwisho huku afisa huo akiwa amesimama wima kila mara akimtishia bi Reynolds
asidhubutu kusongeza mikono yake la sivyo atampiga risasi.
Mwishowe bi Reynolds anakamatwa yeye na mwanawe wanahamishwa
hadi kituo cha polisi.
Video inaonyesha Philando Castile akifuja damu ktoka kifuani
huku polisi mwenye hasira akiwa bado anamuelekezea Bunduki.
Bw Castile, 32, alikuwa msimamizi katika hoteli moja
inayowaandalia watoto wa shule ya Montessori vyakula.
Mpenziwe anasema alikuwa na idhini ya kubeba silaha halali.
Kisa hicho kinatokea huku kiandamana baada ya mauwaji mengine ya
mtu mweusi mjini Lousiana.
Mauaji ya Alton Sterling, yameibua hasira miongoni mwa wenyeji
wa mji huo wa Baton Rouge ambapo Sterling alikuwa akiuza CD.

No comments:
Post a Comment