Msanii aliyewahi kufanya vizuri na wimbo ‘Nimpende Nani’, Voice Wonder
amedai kuwa anajipanga kuvunja ukimya wake wa muda mrefu.
Akiongea na Google In4 kupitia kipindi cha Vibe la Kitaa
cha ABM Radio ya Dodoma kinachoendeshwa na Dj Rodger, Wonder amedai kuwa
hahofii kurudisha tena nafasi yake kimuziki kwakuwa licha ya muziki kubadilika
mchezo anaujua vyema.
Amesema kuwa hakuna anayeweza kubisha kuwa muziki wa
Tanzania umetawaliwa na wasanii wawili tu, akimaanisha Diamond na Alikiba na
kudai kuwa wengi wameshindwa kufikia ukubwa huo.
Pia anadai alichojifunza kwenye muziki wa sasa ni kuwa
idea za nyimbo nyingi zinafanana kuanzia mashairi na melody hivyo hakuna
kinachomshtua.
“Mimi nimefanya muziki kipindi kuna watu wazito na
nikapenya, akina Juma Nature, Inspekta wa moto, Chilla, Bushoke wa mtoto,
Banana, K Bazil na bado unafanya kitu watu wanajua huyu ni Voice, huyu ni
Banana, huyu ni Bushoke kunakuwa na tofauti, mtu anasikia anajua huyu ni fulani
na bado soko halikuwepo gumu kwa upande wangu. Sioni kama kuna wasanii wawili
watatu wanasumbua mimi nikashindwa kupenya pale kati,” amesema.
Muimbaji huyo anayetokea Dodoma, amedai kuwa tayari ana
ngoma tatu ambazo amesharekodi ambazo amewashirikisha Christian Bella, Q-Chief
na Madee.
Amesisitiza kuwa muziki wake sasa hivi una mabadiliko
makubwa kwakuwa amekuwa kimuziki na kiumri.

No comments:
Post a Comment