Ripoti nchini Japan zinasema kuwa
mtu mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi katika kituo hicho cha Tsukui
Yamayuri-en, alijipeleka hadi kituo cha polisi na kukiri kuwa ndiye
aliyetekeleza mauaji hayo ya kutisha na kwa sasa anazuiliwa.
Mtu huo ametambuliwa kama Satoshi
Uematsu, mwenye umri wa miaka 26.
Polisi wanasema mshukiwa alikuwa
amemwandikia barua spika wa bunge la chini mwezi Februari akitishia kuwaua
walemavu.
Alitibiwa hospitali lakini baadaye
akaachiliwa.
Visa vya mauaji ya watu wengi kwa
pamoja huwa nadra sana nchini Japan.
Visa vya watu kuchomwa visu mwaka 2001 na 2008
vilisababisha vifo vya watu saba na wanane mtawalia.
Mwaka 1995, shambulio la kutumia
gesi ya sumu ya sarin katika treni mjini Tokyo, ambalo lilitekelezwa na watu wa
madhehebu ya Aum Shinrikyo, lilisababisha vifo vya watu 12.

No comments:
Post a Comment