
Utafiti mpya umeonesha
kwamba wanaume wa Uholanzi ndio warefu zaidi duniani, na upande wa wanawake,
wanawake wa Latvia ndio warefu zaidi.
Kimo cha wastani kwa
wanaume Uholanzi ni futi 6 kwa sasa (sentimeta 183), na kimo cha wastani kwa
wanawake wa Latvia ni futi 5 inchi 7 (sentimeta 170).
Utafiti huo, ambao
matokeo yake yamechapishwa kwenye jarida la eLife, umefuatilia kimo cha watu na
mabadiliko yaliyotokea katika mataifa 187 tangu 1914.
Utafiti huo umebaini
kwamba wanaume wa Iran na wanawake wa Korea Kusini ndio walioongeza kimo zaidi,
wakiongeza kimo cha wastani kwa zaidi ya inchi 6 (sentimeta 16) na inchi 8
(sentimeta 20) mtawalia.
Wanawake wafupi zaidi
duniani wanapatikana nchini Guatemala huku wanaume wafupi wakitokea Timor
Mashariki.
Mwanamke wa umri wa
miaka 18 kwa wastani nchini Guatemala alikuwa na kimo cha futi 4 inchi 7
(sentimeta 140) mwaka 1914 utafiti wa kwanza ulipofanywa na sasa kiwango hicho
hakijafika kabisa futi 4 inchi 11 (sentimeta 150).
Kimo cha wastani kwa
wanaume Timor Mashariki ni futi 5 inchi 3 (sentimeta 160).
Watafiti hao wanasema
kuwa chembe chembe za jeni hubadilikabadilika, lakini cha muhimu zaidi ni
kuwepo kwa lishe bora, usafi na matibabu ya hali ya juu.
Mataifa yenye wanaume warefu zaidi duniani 2014 (kwenye mabano
ni nafasi iliyoshikiliwa 1914):
1.
Uholanzi (12)
2.
Ubelgiji (33)
3.
Estonia (4)
4.
Latvia (13)
5.
Denmark (9)
6.
Bosnia na Herzegovina (19)
7.
Croatia (22)
8.
Serbia (30)
9.
Iceland (6)
10.
Jamhuri ya Czech (24)
Mataifa yenye wanawake warefu zaidi duniani 2014 (kwenye mabano
ni nafasi iliyoshikiliwa 1914):
1.
Latvia (28)
2.
Uholanzi (38)
3.
Estonia (16)
4.
Jamhuri ya Czech (69)
5.
Serbia (93)
6.
Slovakia (26)
7.
Denmark (11)
8.
Lithuania (41)
9.
Belarus (42)
10.
Ukraine (43)

No comments:
Post a Comment