Wavulana wanne katika shule moja nchini Uingereza wamefika
shuleni wakiwa wamevalia sketi kulalamikia hatua ya mwalimu kuwaadhibu kwa
kuvalia kaptura siku yenye joto kali zaidi nchini humo.
Wanafunzi hao wa darasa la mwaka wa tisa katika shule yaLonghill
eneo la Rottingdean, Sussex Mashariki, walikuwa miongoni mwa wanafunzi 20
wavulana waliovalia kaptura za kuvaliwa wakati wa mazoezi badala ya suruali
ndefu.
Baadhi walifukuzwa shuleni Jumanne na wengine kutengwa hadi siku
iliyofuata. Waliokubali kuvua kaptura hizo na kuvalia suruali ndefu
hawakuadhibiwa.
Lakini badala ya kuvalia sare kamili ya wakati wa masomo, kama
walivyokuwa wameagizwa, wanafunzi wanne walirejea shuleni Alhamisi wakiwa
wamevalia sketi. Watatu waliambia wavue sketi hizo lakini wote kwa pamoja
wakakataa na ndipo wakaruhusiwa kuendelea kukaa shuleni.
Mwalimu mkuu Kate Williams aliwaambia wanaweza kuvalia mavazi
yoyote, mradi yawe ni sehemu ya sare iliyokubalika shuleni.

No comments:
Post a Comment