
Kwamba tarehe 21.08.2016 majira ya
10:00 usiku katika eneo la club ya villa park resort kata ya kirumba wilaya ya
ilemela mkoa wa mwanza, askari namba g.5092 pc john nyange wa ofisi ya mkuu wa
upelelezi na makosa ya jinai mkoa wa mwanza (rco), aliuawa kwa kuchomwa na kitu
chenye ncha kali eneo la shingoni na mtu aliyekuwa anaugomvi nae.
Inadaiwa kuwa marehemu alikua na
ugomvi wa muda mrefu na mtu aliyejulikana kwa jina magina hussein miaka [27]
fundi computer msukuma na mkazi wa mtaa wa kigoto, ambapo marehemu alikuwa
akimdai bwana magina hussein computer aina ya laptop. Ndipo usiku wa leo
majira tajwa hapo juu walikutana eneo la club ya villa park huku mtuhumiwa wa
mauaji hayo ikisemekana kuwa alikuwa na wenzake watano ndipo walimvamia na
kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni na kufariki dunia njiani wakati
akipelekwa hospitali.
Marehemu kwa sasa alikuwa ni
mwanafunzi wa chuo kikuu cha stefano moshi memorial university college cha
mjini moshi, alikuwa anasomea shahada ya sayansi ya habari na mawasiliano mwaka
wa pili, aidha alirejea mwanza baada ya kupata likizo kuja kuiangalia familia
yake ndipo umauti ukamkuta.
Watuhumiwa sita akiwepo magina
selemani ambaye alikuwa na ugomvi na marehemu pamoja na wenzake watano
wamekamatwa, wapo katika mahojiano na jeshi la polisi huku uchunguzi kuhusiana
na kifo hicho ukiwa bado unaendelea, pindi uchunguzi ukikamilika
watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani, mwili wa marehemu umehifadhiwa
hospitali ya rufaa ya bugando kwa uchunguzi.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza
naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wananchi wa jiji na mkoa
wa mwanza, kwamba jeshi la polisi mkoa wa mwanza limesikitishwa na kifo cha
askari huyu kwani limempoteza askari kijana ambaye bado jeshi lilikuwa
linamtegemea.
Lakini pia anawataka watu wenye
tabia za kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga wengine hadi kufikia kupoteza
maisha kuwa wanafanya kosa la jinai, na kama watu wanadaiana wafuate taratibu
za kisheria zilizowekwa ili kuepusha vifo vinavyoweza kuepukika, hivyo jeshi la
polisi linawataka kuacha tabia hiyo mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yao.
Imetolewa na:
Dcp: ahmed msangi
Kamanda wapolisi (m) mwanza

No comments:
Post a Comment