Chris Brown akamatwa na polisi kwa madai ya kumtishia mtu kwa silaha nzito - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 31 August 2016

Chris Brown akamatwa na polisi kwa madai ya kumtishia mtu kwa silaha nzito

   Chris-Brown-2016-ppcorn
Chris Brown amekamatwa na polisi wa LAPD kwa madai kuwa amemtishia mtu kwa silaha nzito.
Baylee Curran alimshutumu Brown kwa kumtishia na bunduki yake huko Tarzana, Calif. Mrembo huyo aliyekuwa akijirusha na Brown kabla ya hapo, anadai kuwa ugomvi ulizuka baada ya kuonesha kutamani midani zake za madini.

Muimbaji huyo alidai kumfukuza msichana huyo na kumtishia na bunduki.
Maofisa wa polisi waliwasili kwenye eneo la tukio saa tisa alfajiri Jumanne hii baada ya simu ya 911 kupigwa na mwanamke aliyehitaji msaada. Curran alipeleka mashtaka polisi na kukatolewa hati ya kufanywa msako.
Wakati wa uchunguzi, Brown anadaiwa kutupa begi lake dogo nje ya dirisa ambamo kulikuwa na bunduki mbili na madawa, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.
Baada ya kulitupa, Breezy anadaiwa kupiga yowe ‘come and get me.’
Kwa sasa amechukuliwa kwenye kitengo cha ‘Robbery Homicide’ kwenye LAPD.

Awali, Brown alitumia Instagram kukanusha madai hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here