Kwa muda sasa mlimbwende wa Tanzania, Hamisa Mobetto amekuwa akituhumiwa
kutaka kumpindua Zari the Bosslady kwa Diamond Platnumz.
Skendo hizo zilivuma zaidi mwezi na kitu uliopita baada
ya kudaiwa kuwa uwepo wa mrembo huyo kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama yake
Diamond kulitaka kusababisha timbwili kwakuwa Zari alikuwepo.
Na sasa Hamisa amefunguka kuwa yeye na Diamond hata
hawajuani kihivyo!
“Hiyo sio kweli,” alisema Hamisa kwenye mahojiano na
gazeti la The Citizen baada ya kuulizwa kuhusu tetesi hizo.
“Pia sijawahi kuwa karibu na Diamond na siku ya kwanza
tumekutana ilikuwa ni siku anazindua video ya Number 1 pale Serena,” aliongeza.
“Tena wakati hiyo habari imeanza kusambaa nilikuwa nje ya nchi.”
Habari hizo zilivuma zaidi wiki kama tatu zilizopita
baada ya kuonekana picha ya Hamisa akiwa kwenye chumba kile kile Diamond
alilala na Zari Afrika Kusini.
Diamond alilazimika kutolea ufafanuzi picha hizo kupitia
kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM. Pia alielezea tetesi za kuwa na uhusiano na
mrembo huyo.
“Hamisa nimeanza kumjua zamani sana na sina uhusiano wa
kimapenzi na yeye, juzi kati alikuwa kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray
Vanny na hiyo ndo imeleta maneno maneno yote hayo,” alisema Diamond.
Na kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia
chumba kimoja alisema, “Pale ni South Africa sehemu ile inaitwa Capital ni
apartment ambazo vyumba vyake vyote vinafanana kama unavyoona hata Madam Rita
pia ana share katika hizo apartment naye anayo yake na pia wabongo wengi
tunapenda kufikia hapo kidogo huwa ni rahisi.”

No comments:
Post a Comment