Waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema viongozi wakuu wastaafu
ambao ni Marais na mawaziri wakuu wamekuwa wakimshauri rais katika masuala
mbalimbali lakini sio katika vyombo vya habari.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
juzi, mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale-Mwiru aliwataka Marais wastaafu na
Mawaziri Wakuu wastaafu nchini kuingilia mvutano wa kisiasa unaoendelea.
Warioba amemjibu Kingunge akisema,”Kweli tuko kimya
lakini ukimya huo usitafsiriwe vibaya kuwa hatumshauri Rais Magufuli, sisi kama
viongozi wastaafu tunamshhauri rais lakini sio katika vyombo vya habari.”
“Badala ya kumjibu Kingunge ni vyema kumuachia Msajili
wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi awakutanishe viongozi wa vyama vya
siasa kujadili hali hiyo kwa lengo la kupata muafaka”, aliongezea.
“Ni wajibu wa Watanzania wote kuhakikisha wanalinda hali
ya amani nchini badala ya kuliona jambo hilo, na kusema jambo hili halimhusu
Rais John Magufuli pekee linamhusu mtu mwingine yeyote. Tumsaidie msajili
katika hili, hili sio tatizo la mtu mmoja bali ni la nchi nzima, tusimuachie
Rais wetu.”
BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:
Post a Comment