Mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda, amefafanua juu ya kauli yake aliyoitoa hivi karibuni
ambayo imekuwa ikinukuliwa vibaya na vyombo vya habari ikiwemo gazeti la leo la
Mwananchi.
Kwenye
ukurasa wa tatu, gazeti hilo limeandika habari yenye kichwa kinachosomeka,
“Makonda ataka wahalifu wagongwe, wapigwe.”
Akiongea
na Clouds 360 ya Clouds FM, Makonda amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanapenda
kuwagombanisha wananchi na viongozi wao kutokana na kauli wanazozinukuu kutoka
kwao.
“Unajua
kuna baadhi ya wenzetu wana agenda zao tofauti na agenda ya kujenga taifa, watu
ambao wangependa kuwatengenezea mazingira wananchi wasielewane na viongozi
wao,” amesema Makonda.
“Kwa
sababu ukiangalia hii stori ilivyoandikwa kuna kitu kimewekwa ambacho hakipo
kabisa lakini kimewekwa kwa tafsiri ya kumsaidia mwenye kusudi la kufikisha
ujumbe tofauti na ule uliotolewa,” ameongeza.
Aidha
Makonda ameendelea kwa kufafanua kauli yake hiyo iliyonukuliwa vibaya kwa kudai
kuwa, “unapokuwa msituni ni sawa na mapambano lazima upambane kwa kuwalinda
polisi wako, majambazi siyo watu wazuri kutokana na tukio lililotokea la kuuawa
kwa polisi wanne hivi karibuni.”

No comments:
Post a Comment