
Waziri wa Ujenzi Prof. Makame
Mbarawa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege ATCL
Kapten Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji Kapten Sadick Muze kwa kosa
la kumchagua rubani asiye na sifa kwenda kupata mafunzo Canada.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri
Mbarawa amesema marubani watano walichaguliwa kwenda nchini Canada kwa ajili ya
kupata mafunzo ya kurusha ndege mpya zitakazoingia nchini mwezi Septemba kama
alivyoahidi Rais Dkt. John Magufuli.
Waziri ameongeza kuwa baada ya
kukamilika kwa malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya za shirika la
ATCL alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi huyo kuchagua marubani watano wenye
sifa kwa ajili ya kwenda kupata mafunzo nchini Canada ambapo kati ya watano
waliochaguliwa mmoja amebainika hana vigezo hivyo ameamua kuwasimamisha
viongozi hao kutokana na uzembe.
Aidha waziri Mbarawa amewataka
watendaji wa serikali kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kanuni za
kazi na mtumishi atakayefanya kinyume hatasalimika kuwajibishwa.

No comments:
Post a Comment