
JESHI la Polisi, Mkoa wa
Kilimanjaro, linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye
umri wa miaka 12.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa
Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa, aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba
aliyebakwa ni mwanafunzi wa darasa la tano na ana umri wa miaka 12.
Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa,
mtuhumiwa huyo ambaye ni mlinzi, Philipo Stephano , alikamatwa Agosti 2 mwaka
huu, saa tisa mchana katika maeneo ya Soweto, Kata ya Soweto, Manispaa ya Moshi
mkoani hapa.
“Yule mtoto ambaye jina lake
tunalihifadhi, alibakwa na babu yake mzaa mama yake, mkazi wa Soweto.
“Kabla ya mtuhumiwa kufanya tendo
hilo, alimwambia mjukuu wake huyo amwelekeze na alipokubali, alimpeleka katika
eneo analolinda na kumfanyia unyama huo.
“Baada ya uchunguzi wa daktari,
ilithibitika mwanafunzi huyo alibakwa na kusababishiwa maumivu makali katika
sehemu zake za siri.
“Kwa hiyo, mtuhumiwa tumemkamata na
tunaendelea na upelelezi kabla hatujampeleka katika vyombo vya sheria,” alisema
Kamanda Mutafungwa.
No comments:
Post a Comment