Makamanda wengine wakuu wa kundi hilo pia wameuawa.
Taarifa kutoka kwa jeshi la angani la Nigeria imesema shambulio
hilo lilitekelezwa Ijumaa tarehe 19 Agosti viongozi hao walipokuwa wakishiriki
sala ya Ijumaa katika kijiji cha Taye, eneo la Gombale katika msitu wa Sambisa
jimbo la Borno.
Kwa mujibu wa jeshi, makamanda ambao wameuawa ni pamoja na
Abubakar Mubi, Malam Nuhu na Malam Hamman.
"Kiongozi wao, anayefahamika kama, "Abubakar
Shekau", anaaminika kujeruhiwa vibaya begani," jeshi limesema kupitia
taarifa iliyotolewa na naibu mkuu wa mawasiliano Kanali Sani Kukasheka Usman.
Kundi la Boko Haram karibuni limekabiliwa na mzozo wa uongozi.
Kundi
la Islamic State lilitangaza kwamba Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa
Boko Haram.
Lakini muda mfupi baadaye, Shekau alisema kuwa bado ndiye
anayeliongoza kundi hilo na akamshtumu al-Barnawi kwa kujaribu kufanya
mapinduzi dhidi yake.
No comments:
Post a Comment