GHENT, Ubeligiji
WATUMIAJI wa pombe sasa wataweza
kupata auheni ya bei ya vinywaji hivyo, baada ya wanasayansi kugundua kifaa
maalumu kitakachotumika kubadilisha mikojo ya walevi kutumika kutengenezea bia.
Kugunduliwa kwa kifaa hicho ni
mkombozi kwa wamiliki wa viwanda vya pombe ambapo wataweza kupata malighafi ya
kutengenezea bia kwa urais.
Kinatarajiwa kufungwa kwenye vyoo
vya baa mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa mikojo hiyo ya walevi.
Kifaa hicho ambacho kitakuwa
kikitumia umeme wa jua pia kitakuwa na uwezo wa kubadili mikojo hiyo kutumika
kama maji ya kunywa.
Timu ya watafiti kutoka Chuo Kikuu
cha Ghent nchini Ubeligiji, walisema kifaa hicho kitaanza kutumika hususan
maeneo ya mijini kwenye nchi zinazoendelea.
Licha ya kuwepo kwa mashine maalum
yenye uwezo wa kutibu maji machafu ikiwemo mkojo kisha kutumika kwa matumizi
mengine muhimu ya binaadamu, wataalamu hao wamesema kifaa hicho walichokigundua
kinauwezo zaidi wa kuyatibu maji hayo bila kutumia nguvu ya umeme.
Dk. Sebastiaan Derese, alisema
kifaa hicho kitakuwa kikitunza mikojo kwenye tangi maalum ambalo litatumika
kutibu kisha kutumika kama malighafi ya kutengenezea bia.
Kwa mara ya kwanza kifaa hicho
kilianza kutumika kwenye tamasha la muziki ililofanyika mjini humo ambapo jumla
ya lita 1000 za mikojo, zilikusanywa kisha kutengenezewa bia.
Alibainisha kuwa, bia
zilizotengenezwa kupitia mikojo hiyo imewavutia wanywaji wengi hususan kwenye
matamasha mbalimbali.
No comments:
Post a Comment