Mr Blue amekiri kuwa
skendo yake kuwa amekuwa akiwasiliana na ex wake, Naj ambaye kwa sasa ana
uhusiano na Barakah Da Prince ilitaka kuivunja ndoa yake.
Akiongea
na Clouds FM, rapper huyo wa ‘Mboga Saba’ amedai kuwa mke wake, Wahyda sasa
amekuwa na wivu wa kufa mtu tangu kuzuke skendo hiyo.
“Sasa
hivi naona kama wivu umezidi baada ya hii skendo ya hawa jamaa kuitengenezea
kiki kwasababu wanataka kutoa nyimbo yao, skendo kwamba mimi nilimpigia yule
mwanamke mwingine nani anaitwa, Najma yule.
Wametengeneza
kweli kabisa, mimi nimezipata za kunyapianyapia kwamba wametengeneza ili
kukikisha nyimbo zao,” amesema Blue.
“Lakini wamenikosea sana kwasababu wanataka kugombanisha ndoa yangu,
mimi nina mke ujue, siwezi kumpigia mtu ambaye nimemwacha, ni kosa kubwa sana,
halafu mke wangu yule ni mwanamke ambaye walikuwa watatu kupigania nani awe na
mimi, yaani bora hata ningempigia mtu mwingine,” amesisitiza.
“Ilifika karibu kama siku mbili tuna ugomvi mimi na mke
wangu, ni kitu kikubwa sana, nimekasirika sana, nimechukia sana na nawaambia
mashabiki wangu, alichokifanya Barakah na watu wake, kama sio yeye simlaumu,
kama watu wake nilikuwa naomba waoneshe proof kwenye mitandao waoneshe namba
yangu niliyompigia, waioneshe kwamba ni hiyo kweli sio unaongeaongea tu.”
Skendo hiyo ilianza baada ya Barakah kudaiwa kushika simu ya mpenzi wake
Naj, alipiga mtu ambaye namba yake ‘iliseviwa’ Zai na baada ya
Barakah kupokea alikuta sio mwanamke bali ni mwanaume ambaye alidaiwa kuwa ni
Mr Blue.

No comments:
Post a Comment