Ofisi za Bunge zilizopo Jijini Dar
es salaam zinatarajia kuhamishiwa Dodoma mwezi Septemba mwaka huu, ikiwa ni
utekelezaji wa agiza la Rais Magufuli la kuhamishia shughuli za serikali
Dodoma.
Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa
Bunge, Job Ndugai jana na kusema kuwa kwa bunge suala la luhamia
Dodoma siyo gumu kwa kuwa tayari makao makuu yake yako Dodoma.
Alisema tayari alikwishatoa maagizo
kwa ofisi yake kuhakikisha kuwa kufikia mwezi Septemba kila kitu kinachofanyika
Dar es salaam kifanyike Dodoma isipokuwa mambo machache.
"Nimeagiza ofisi yangu ihamie
dodoma mara moja kuanzia Septemba hii, watumishi wa bunge karibu wote watahamia
Dodoma, masuala ya malipo yataangaliwa baadaye, kwa sasa ni kuhamia dodoma tu,
ofisi tunazo huko" Alisema Ndugai
Kama sehemu ya mwanzo wa
utekelezaji wa azma hiyo, tayari ofisi ya bunge imetangaza kufanyia Dodoma
vikao vyake vyote vya kamati za bunge tofauti na ilivyokuwa umepangwa mwanzo na
ilivyozoeleka kufanyikia Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment