
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda amewapiga marufuku mawakala wanaotoza faini za kuegesha magari vibaya
katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo hadi hapo
yatakapotengenezwa maeneo rasmi kwa ajili ya maegesho ya magari.
Makonda alitoa kauli hiyo jana
wakati alipofanya ziara kujionea hali halisi ya kituo hicho.
Alisema haiwezekani mawakala
wakaendelea kutoza faini za maegesho ambayo si sahihi wakati katika eneo hilo
hakuna maeneo maalumu kwa ajili ya maegesho ya magari.
“Nataka maeneo
rasmi yakishatengwa ndipo muanze kutoza faini, mmekuwa mkiwasumbua wananchi
hawajui wapi ni sehemu ya maegesho na wapi si sehemu ya maegesho wekeni alama
ndipo muanze kuwatoza,” alisema Makonda.
Licha ya kutoa kauli hiyo, Makonda
pia alimtaka Mkurugenzi wa Jiji kabla ya kumalizika wiki hii kuhakikisha kituo
hicho kinawekwa taa ili kuondoa usumbufu wanaokutana nao abiria na wananchi
hasa wakati za usiku.
"Lakini kabla ya wiki hii
haijaisha nataka kuona taa zote za ubungo zinawaka, sitaki kuviona vifusi
katika eneo hili la stendi na baada ya siku 20 nitarejea kujionea utekelezaji
wake kama umekamilika" Alisema Makonda
Katika hatua nyingine, Makonda
alisema kuwa serikali ipo katika mpango mwisho wa kuihamishia stendi hiyo
kutoka ubungo kwenda Mbezi mwisho.
"Shahuku
yangu ni kuwa na stendi tofauti na tuliyonayo, nataka Dar es salaam iwe na
stendi ya kimataifa na tayari tunalo eneo kule mbezi ambapo halmashauri ya jiji
tayari ipo kwenye mchakato wa kukamilisha ujenzi huo.
"Nataka
kuihamisha hii stendi ya ubungo ili tuepukane na kero ya kukutana na mabasi ya
mwendo kasi kwakuwa nayo ni moja ya changamoto, duniani kote maroli
yakiingia katikati ya mji hutumika kubeba mikate ajabu Dar es salaam maroli
yanabeba ngano na makontena"

No comments:
Post a Comment