Lakini mmoja alionekana kuwasisimua watazamaji zaidi ya wengine.
Alikuwa ni Pita Nikolas Taufatofua, mwanamichezo kutoka Tonda
ambaye alikuwa kifua wazi na chini amevalia vazi la kitamaduni la Tonga, kwa
jina ta'ovala.
Taufatofua, alizaliwa Australia lakini akalelewa Tonga.
Ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tonga kuwakilisha taifa hilo
katika mchezo wa taekwondo. Yeye huishi Brisbane ambapo huwasaidia watoto wasio
na makao.
Kwa mujibu wa tovuti ya USA Today, mwanataekwondo huyo wa umri
wa miaka 32 alijaribu kufuzu kwa Olimpiki mara mbili awali.
Atashindana
katika kitengo cha wanaume wa uzani wa kilo 80 na zaidi Jumamosi tarehe 20
Agosti.
Ni mmoja kati ya wachezaji saba wanaowakilisha taifa hilo la
Polynesia linalotawaliwa na ufalme katika Michezo ya Rio.
Tonga imeshinda nishani moja pekee katika historia yake, medali
ya fedha mwaka 1996.

No comments:
Post a Comment