Msanii
wa muziki, Linah Sanga amekanusha tetesi ambazo zilisambaa katika mitandao ya
kijamii kuwa anatoka kimapenzi na rapper Billnas.
Muimbaji
huyo ambaye ameachia wimbo ‘Raha Jipe Mwenyewe’ hivi karibuni, amekiambia
kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa Billnas ni mshkaji wake.
“Watu
wanatakiwa wajue tu kuwa mimi na BillNas si wapenzi ila sisi ni watu wa karibu
sana,” alisema Linah “Saizi mimi na Bill Nas ni washikaji sana maana siri yake
ndiyo siri yangu,”
Aliongeza,
“Bill Nas ndiye aliyenishauri nibadilike kwenye muziki na kunipa ‘connection’
na ‘Producer’ T Touch, yeye ndiye aliniambia nibadili mfumo mzima wa muziki
wangu na ndiyo nikafanya hivyo,”

No comments:
Post a Comment