Mgombea
Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump amebadilisha
mwelekeo wa kampeni zake na kujikita kwenye masuala ya uchumi baada ya wiki
ngumu ya kuanza kampeni za uchaguzi.Trump akiwa mjini Detroit ameahidi kuibua
uchumi wa Marekani kwa mwendo wa kasi kwa kufuta kodi za mashirika endapo
atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo mwezi Novemba.
Amesema nafasi nyingi
za kazi zitatengenezwa kwa mabadiliko hayo ya mfumo wa kodi sanjari na
makubaliano mapya ya mkataba wa kibiashara wa kanda ya Marekani ya Kaskazini.
Mabadiliko niliyoyaelezea leo ni ya mwanzo tu. Tutakapofanya
mabadiliko katika mfumo wetu wa kodi, biashara, nishati na sera za uthibiti,
tutakuwa tumefungua ukurasa mpya kabisa, tutakuwa tumefungua ukurasa mpya
katika maendeleo ya Marekani, ambayo yanahitajika sana. Tunahitaji ukurasa
mpya.Donald Trump, Mgombea Urais wa Marekani-Republican
Trump amesema
kupunguza kodi ndio itakuwa kitovu cha mipango yake ya kuhuisha uchumi wa
Marekani, iwapo atashinda katika uchaguzi wa Novemba.
Katika hotuba yake
kubwa ya sera za uchumi aliyoitoa mjini Detroit, huku akikatishwa mara kwa mara
na kelele za waandamanaji,Trump amesema kiwango cha kodi kwa wafanya kazi
kitakuwa kidogo mno hivyo kuzalishwa kwa mamilioni ya kazi. Amesema anataka
kufungua ukurasa mpya kwa uchumi wa Marekani.
Nae mgombea urais
kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton akihutubia mkutano mjini Florida,
amekosoa mikakati ya bwana Trump na kusema katu haitasaidia idadi kubwa ya
wamarekani, lakini inasaidia watu ambao tayari wap juu.
Wakati huo huo, msuguano mkali
umeendelea baina ya Maafisa
hao akiwemo mkurugenzi wa zamani wa CIA na mawaziri wawili wa mambo ya ndani,
wametoa taarifa inayo mtuhumu Trump kwa kukosa uwezo, haiba na uzoefu wa
kuhudumu kama rais wa Marekani. Wamebashiri kuwa huenda akawa Rais asiye na
uwezo kwenye historia ya Marekani tangu taifa hilo kuanzishwa.
Wakati huo huo, msuguano mkali
umeendelea baina ya Maafisa
hao akiwemo mkurugenzi wa zamani wa CIA na mawaziri wawili wa mambo ya ndani,
wametoa taarifa inayo mtuhumu Trump kwa kukosa uwezo, haiba na uzoefu wa
kuhudumu kama rais wa Marekani. Wamebashiri kuwa huenda akawa Rais asiye na
uwezo kwenye historia ya Marekani tangu taifa hilo kuanzishwa.

No comments:
Post a Comment