Mambo mengi yametokea wiki hii kuanzia Wema Sepetu kuachana na mpenzi
wake Idris Sultan hadi Miss Tanzania huyo wa mwaka 2016 kuhudhuria birthday
party ya binamu wa Diamond, Romeo na kukutana na vijana wa WCB.
Kutokana na Wema kujumuika na vijana wa himaya ya WCB,
kumezuka tetesi kuwa huenda ukaribu kati ya muigizaji huyo na Diamond unaweza
ukawa ni zaidi ya maex wawili walioamua kuacha bifu zao zipite.
“Yaani watu wakianza tu kuongea vizuri, bifu zao
zikiisha wamerudiana, maisha lazima yaendelee, mwisho wa siku hatuwezi kuwa
tunakaa tunachuniana miaka yote tutakayoishi, life is too short,” Wema
alimweleza Soudy Brown kupitia U Heard ya Clouds FM.
“Mimi mwenyewe najisikia hadi amani kwamba there is no
beef, maisha yanaendelea, mimi sijarudiana na Diamond, mimi namrespect kama
msanii, nampenda Diamond kama msanii and I love his music and I am so glad
tumeweka all this behind,” aliongeza.
Kuhusu kama anampenda mtoto wa Diamond, Tiffah, Wema
alisema, “Tiffah amenikosea nini katika maisha yangu? Nimchukie Tiffah si
nitakuwa mwendawazimu jamani,” alisisitiza.
Kuhusu tetesi kuwa aliwahi kumuita Tiffah zombie kama
Zari alivyowahi kudai lakini Wema amezikanusha, “Hayo maneno sio ya kwangu,
sijawahi hata siku moja, kwanza the way I adore babies, siwezi nikamuita baby
zombie hata awe vipi.”
Kuhusu Zari staa huyo alisisitiza kuwa hana bifu naye.
“Mimi sina bifu na Zari na sijawahi kuwa na bifu na
mwanamke wake yeyote Nasib, kwasababu huwa naona matatizo yangu mimi na Nasib
ni mimi na yeye, Zari hana makosa, katongozwa, amedetiwa, amewekwa ndani, hana
makosa hata kidogo huyo mwanamke.”

No comments:
Post a Comment