Mchezaji wa Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa Agosti 18 amefanikiwa
kuifungia timu yake ya KRC Genk goli moja kwenye mchezo wa UEFA Europa League
waliocheza dhidi ya Locomotiva Zagreb ya Croatia.
Kwenye mchezo huo wa kuwania kupangwa kwenye hatua ya
makundi timu hizo zilifanikiwa kutoka sare ya kufungana goli 2-2.
KRC Genk ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao kwa njia ya
Penalti kupitia kwa mchezaji wake raia wa Ubelgiji, Leon Bailey huku Samatta
akiifungia timu yake hiyo bao la pili dakika ya 47.
Zagreb ambao walikuwa
nyumbani walifanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia kwa Mirko Marić kwa njia
ya penalti dakika ya 52 na dakika ya 59 goli likifungwa na Ivan Fiolić.
Timu hizo zinatarajiwa kurudiana tena Agosti 25 mwaka
huu kwenye uwanja wa Cristal Arena unaomilikiwa na timu ya KRC Genk huku timu
hiyo ikihitaji sare yoyote isiyozidi bao moja ili ipate nafasi ya kusonga
mbele.

No comments:
Post a Comment