Habari za kufikiwa kwa makubaliano
hayo zimesababisha kupanda kwa bei ya mafuta ghafi kwa karibu asilimia 6.
Wanachama wa Opec wamekuwa
wakilaumiana kusababisha mdororo wa bei ya mafuta kutoka nana wao kushindwa
kuchukua msimamo mmoja wa kudhibiti bei.
Wanachama wa Opec wamekuwa
wakikutana Algeria.
"Opec imechukua uamuzi wa
kipekee leo," waziri wa mafuta wa Iran Bijan Zanganeh amesema.
Mafuta ghafi ya Brent, yanayotumiwa
kama kigezo cha amfuta kimataifa, yalipanda bei na kufikia karibu asilimia 6
hadi $49 kila pipa baada ya tangazo hilo kutolewa.
Mawaziri wa mafuta wa nchi
wanachama wamesema maelezo ya kina kuhusu mwafaka wa sasa yatajadiliwa kwenye
mkutano mwingine Novemba.
Uzalishaji wa mafuta utapunguzwa
hadi mapipa 700,000 kwa siku, ingawa upunguzaji wa uzalishaji hautakuwa sawa
miongoni mwa wanachama.
Iran itaruhusiwa kuongeza
uzalishaji wake.
Kulikuwa na suitafahamu awali baina
ya Iran na mpinzani wake Mashariki ya Kati Saudi Arabia, jambo ambalo lilikuwa
limezuia kupatikana kwa mwafaka.
Wazalishaji wadogo wa mafuta walipigania kupunguzwa kwa
uzalishaji baada ya mafuta kushuka bei kutoka $110 miaka miwili iliyopita.
Waziri wa mafuta wa Nigeria Ibe
Kachikwu, taifa lililoathirika sana, alisema huo ni "mkataba mzuri
sana".
Waziri wa kawi wa Algeria Algerian
Noureddine Bouarfaa amesema uamuzi huo huo ulifikiwa kwa kauli moja.
Waziri wa kawi wa Qatar Mohammed
Bin Saleh Al-Sada ambaye ndiye rais wa sasa wa Opec amesema uzalishaji sasa
utakuwa kati ya mapipa 33.2 milioni na 33 milioni kwa siku.
Uzalishaji wa sasa unakadiriwa kuwa
mapipa 33.3 milioni kwa siku.
No comments:
Post a Comment