Chris
Brown yupo nje kwa dhamana.
Muimbaji
huyo ametoka kwa dhamana ya $250,000 usiku wa Jumanne baada ya kukamatwa kwa
madai ya kumtishia mtu na silaha.
Baylee
Curran alimshutumu Brown kwa kumtishia na bunduki yake huko Tarzana, Calif.
Mrembo huyo aliyekuwa akijirusha na Brown kabla ya hapo, anadai kuwa ugomvi
ulizuka baada ya kuonesha kutamani midani zake za madini.
Muimbaji
huyo alidaiwa kumfukuza msichana huyo na kumtishia na bunduki.
Maofisa
wa polisi waliwasili kwenye eneo la tukio saa tisa alfajiri Jumanne hii baada
ya simu ya 911 kupigwa na mwanamke aliyehitaji msaada. Curran alipeleka
mashtaka polisi na kukatolewa hati ya kufanywa msako.
Wakati
wa uchunguzi, Brown anadaiwa kutupa begi lake dogo nje ya dirisa ambamo
kulikuwa na bunduki mbili na madawa, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.
Baada
ya kulitupa, Breezy anadaiwa kupiga yowe ‘come and get me.’
Brown
atapanda kizimbani Sept. 20 na bado anakana mashtaka hayo.

No comments:
Post a Comment