Rais wa Sudan Kusini
hatimaye amekubali kikosi cha ziada cha wanajeshi wa kulinda amani kitumwe
nchini humo.
Rais Salva Kiir
alichukua hatua hiyo baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kwa Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa.
Bw Kiir alikuwa awali
amekataa kutumwa kwa wanajeshi hao 4,000 kutoka mataifa ya kanda, akisema huo
ni ukiukaji wa uhuru wa Sudan Kusini.
UN iliidhinisha
kutumwa kwa wanajeshi hao baada ya kuzuka upya kwa vita baina ya wanajeshi
waaminifu kwa Bw Kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Dkt Riek Machar mwezi
Julai mjini Juba.
Kikosi hicho cha ziada
kitakuwa na mamlaka zaidi kushinda kikosi cha sasa cha wanajeshi 13,000 ambacho
kimekuwa kikihudumu nchini humo.

No comments:
Post a Comment