Mr Blue amesema kwa
sasa amekuwa mtu mzima na kwamba mambo ya kupiga pamba kama zamani amewaachia
wasanii vijana zaidi.
Akiongea
na Clouds Fm, rapper huyo amesema kama mke wake atapenda anachovaa, hakuna
kinachompa mawazo tena.
“Unajua
unapokuwa pia na mambo nayo yanabadilika, najitahidi sasa hivi navaa simple,
lakini nimependeza siwezi tena kuvaa yale manguo sijui makubwa au unikute
nimevaa kijinsi sijui kimenibana au kipo kama sketi siwezi,” alisema.
“Na
wala huwa sina sijui role model, nikienda dukani hiki kizuri navaa. Mke wangu
ambaye ndio nimemuoa akiniambia yeye nimependeza inatosha kabisa, hata kama
nimevaa taulo natoka nalo tu mambo ya kwenda na wakati sasa nawaachia wadogo
zangu kama akina Young Killer, Jux,” alisisitiza Blue.

No comments:
Post a Comment