Watumishi 34 wa mahakama nchini, wamefukuzwa kazi baada ya tume ya
maadili utumishi wa mahakama kujiridhisha kuwa wamekiuka sheria na taratibu za
kazi wakati wakitimiza majukumu yao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othumani, alitoa sababu za watumishi hao
kupumzishwa, “Sababu ya makosa kinidhamu, kuna mmoja yeye alitumia muhuri wa
mahakama kinyume cha taratibu na sheria za mahakama.”
Pia jaji Othuman alibainisha mpango wa kuwawezesha
wananchi kutoa taarifa kwa watendaji kazi wa mahakama.
“Kwahiyo kila wilaya kama mtakavyoona hapa Dar es
Salaam, kuna namba maalum Kinondoni, kuna namba maalum Temeke,na kuna namba
moja ile ya taifa tutapata hapa taarifa juu ya hayo mapendekezo au maoni na
malalamiko.”
BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:
Post a Comment